Kampuni ya Denmark yatarajia ushirikiano na suluhu za kijani katika CIIE

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2024

Skrini inayotangaza Maonyesho yajayo ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ikionekana katika picha kwenye lango la kuingia la Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano (Shanghai), ukumbi mkuu wa CIIE, mjini Shanghai, mashariki mwa China, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Fang Zhe)

OSLO – Huku Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yakikaribia, Danfoss, kampuni ongozi ya Denmark ya suluhu fanisi ya nishati, inajiandaa kuonyesha bidhaa zake zenye uvumbuzi na kutangaza ushirikiano mpya wa kimkakati unaolenga kutoa mchango katika kubadili muundo wa uchumi wa China kuwa wa kijani.

Mwaka huu itakuwa ni mara ya tano kwa Danfoss kushiriki katika CIIE, na uongozi wa kampuni hiyo una matumaini kuhusu fursa ambazo maonyesho hayo yanawasilisha.

Kim Fausing, Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Danfoss, amesisitiza umuhimu wa CIIE katika kuhimiza ushirikiano na ukuaji wa biashara.

"Kupitia ushirikiano mpya tutakaotangaza wakati wa CIIE, tunatumai kuendeleza kwa kasi utekelezaji wa suluhu zetu za kijani. Ujumbe wetu uko wazi: haiwezekani tu kuzuia utoaji wa hewa chafu kwa teknolojia iliyopo ya kuondoa kaboni, lakini pia ina faida," Fausing ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Wafanyakazi wakiandaa ukumbi kwa ajili ya Maonyesho yajayo ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) kwenye Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano (Shanghai), mjini Shanghai, mashariki mwa China, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Fang Zhe)

Akisisitiza kwamba CIIE ni jukwaa muhimu kwa kampuni za kimataifa kutafuta fursa katika uchumi wa kijani unaokua kwa kasi nchini China, amesema kuwa Danfoss inaweza kutoa mchango katika ajenda ya kijani ya China.

"CIIE ni jukwaa bora kwetu kuelewa vyema soko la China na kuimarisha uhusiano wetu na washirika wetu wa China," Fausing amebainisha.

Mwaka huu, Danfoss italeta suluhu pana kwenye CIIE, unaojumuisha sekta kama vile vituo vya data, kutibu maji safi na maji taka, na sekta ya chakula na vinywaji baridi. Fausing amesisitiza kuwa suluhu hizo zimeundwa ili kuleta thamani ya kipekee kwa China kubadilisha muundo wake wa uchumi kuwa wa kijani, zikitoa ufanisi na uendelevu.

Maonyesho ya 7 ya CIIE, yaliyopangwa kufanyika Shanghai kuanzia Novemba 5 hadi 10, yamevutia washiriki kutoka nchi, kanda na mashirika ya kimataifa 152, na yameweka rekodi mpya kwa viongozi 297 wa Kampuni Bora 500 Duniani kupanga kushiriki.

Picha hii ikionyesha mwonekano wa Kituo cha Taifa cha Maonyesho na Mikutano (Shanghai), ukumbi mkuu kwa ajili ya Maonyesho yajayo ya 7 ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) mjini Shanghai, mashariki mwa China, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Fang Zhe)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha