

Lugha Nyingine
Botswana yakabidhiwa shule ya nne ya msingi iliyojengwa kwa msaada wa China
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi (pili kulia) na Balozi wa China nchini Botswana (kwanza kushoto) wakizindua shule ya msingi ya Ramaeba. (Picha/Xinhua)
Botswana imekabidhiwa rasmi shule ya msingi ya nne siku ya Jumapili iliyojengwa kwa msaada wa China.
Shule hiyo ya msingi ya Ramaeba iliyopo kijiji cha Kazungula, kaskazini mwa Botswana, imejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba takriban elfu 61 ambapo ndani yake kuna madarasa 14 yanayoweza kuchukua wanafunzi 560, majengo 16 yanayojumuisha jengo la kufundishia, ofisi, maktaba, mgahawa, bweni la walimu na uwanja wa michezo.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya shule hiyo, Balozi wa China nchini Botswana Bw. Fan Yong amesema China imetambua kuwa elimu ni kitu muhimu zaidi kwenye mchakato wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Botswana.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa na Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana, Makamu wa Rais Slumber Tsogwane na maofisa wengine wa ngazi ya juu.
Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo ya uzinduzi, Makamu wa Rais Tsogwane amesisitiza kuwa mafanikio hayo ni ushahidi wa ushirikiano imara kati ya Botswana na China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma