Botswana yazindua boti ya umeme ambayo ni rafiki kwa mazingira ili kuboresha mpango wa usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme

(CRI Online) Oktoba 28, 2024

Botswana imezindua rasmi ubunifu wake mpya wa usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme, yaani Boti inayotumia Umeme (eBoat), ikiashiria hatua muhimu katika azma yake ya kufikia usafiri wa vyombo vinavyotumia umeme.

Mpango huo ni nyongeza katika bidhaa mfululizo za usafiri wa kijani ziliozinduliwa na serikali katika wiki za karibuni, kama ilivyosisitizwa na Rais Mokgweetsi Masisi katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Makamu wa Rais Slumber Tsogwane siku ya Jumapili kwenye hafla ya uzinduzi iliyofanyika kitongoji cha mapumziko cha Kasane kilichopo kaskazini-magharibi mwa Botswana.

Tsogwane amesema Botswana inaendana na malengo yaliyoainishwa katika Mkakati wake wa Kuhamia Nishati Mbadala, unaolenga kuongeza matumizi ya vyanzo vya nishati safi katika sekta mbalimbali, ikiwemo uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma.

Mapema mwezi huu, Botswana ilizindua magari yake ya kwanza yanayotumia umeme yaliyounganishwa sehemu zake mjini Gaborone, kwa uungaji mkono wa kampuni mbili za utengenezaji magari za China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha