Rais Xi Jinping asisitiza kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu za kitamaduni ifikapo Mwaka 2035

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2024

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu amesisitiza kuelekeza jitihada katika kuijenga nchi ya China kuwa yenye nguvu katika utamaduni ifikapo Mwaka 2035.

Akiendesha semina elekezi ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC uliofanyika jumatatu, Rais Xi amesisitiza kuendeleza kila wakati utamaduni wa ujamaa wenye umaalum wa China katika zama mpya.

Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kuendelea kufuata Umarksi kama kanuni elekezi ya kimsingi, kukita mizizi katika ustaarabu mpana na wa kina wa China, na kuendana na mwelekeo wa kuendelea wa teknolojia ya habari.

Rais Xi amesisitiza kuendeleza utamaduni wa kijamaa wenye nguvu kubwa ili kuongoza nadharia, kuunganisha na kuhamasisha watu, na kuwa na ushawishi duniani.

"Tumeweka uendelezaji wa utamaduni kwenye nafasi muhimu katika kutawala nchi tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC ulipofanyika," amesema Rais Xi, na aliongeza kuwa mfululizo wa mipangilio mikuu imefanyika, ikiunda mawazo juu ya utamaduni wa ujamaa wenye umaalum wa China katika zama mpya.

Pia ametambua mafanikio madhubuti yaliyopatikana katika kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu katika utamaduni.

Rais Xi pia amesisitiza umuhimu wa kufuata uongozi wa Chama, kuinua uwezo wa utawala katika sekta ya utamaduni katika mazingira ya teknolojia ya habari, na kufuata mwongozo wa maadili ya msingi ya ujamaa.

Akisisitiza umuhimu wa kuhamasisha ubunifu wa kitamaduni wa taifa zima, Rais Xi ametoa wito kwa juhudi za kuhimiza demokrasia kikamilifu katika utafiti wa kitaaluma na shughuli za kisanii, na kutoa uungaji mkono kwa waandishi, wasanii na wasomi kupata hamasa kutokana na maisha ya kila siku na kujikita katika kubuni.

Ametoa wito kwa juhudi za kukidhi mahitaji mbalimbali ya kiutamaduni ya umma katika ngazi tofauti na katika nyanja mbalimbali, na kuongeza uwezo wa utoaji wa huduma na bidhaa za kitamaduni.

Rais Xi pia amesisitiza umuhimu wa kuhimiza urithishaji wa kitamaduni wa China kupitia mageuzi na maendeleo ya kibunifu.

Akisisitiza haja ya kuboresha nguvu laini ya utamaduni ya China na mvuto wa utamaduni wa China, Rais Xi ametoa wito wa juhudi za kufanya mawasiliano na ushirikiano zaidi wa kimataifa wa kati ya watu, na kujifunza kutokana na mafanikio makubwa ya staarabu zote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha