Idadi ya Wapalestina waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel mjini Gaza yazidi 43,000

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 29, 2024

Mtu akiangalia hali ya uharibifu baada ya shambulizi la Israeli dhidi ya kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

Mtu akiangalia hali ya uharibifu baada ya shambulizi la Israeli dhidi ya kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

GAZA - Idadi ya Wapalestina waliofariki kutokana na mashambulizi yanayoendelea ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza imefikia 43,000, idara ya afya ya Gaza imesema katika taarifa yake siku ya Jumatatu ikiongeza kuwa katika muda wa saa 48 zilizopita, Jeshi la Israel limewaua watu 96 na kuwajeruhi wengine 277, ikifanya idadi ya vifo kufikia 43,020 na majeruhi kufikia 101,110 tangu mgogoro kati ya Palestina na Israel kuzuka mapema Oktoba 2023.

Waathiriwa kadhaa bado walikuwa chini ya vifusi, na ambulensi na timu za ulinzi wa raia hazikuweza kuwafikia, imesema taarifa hiyo.

Jeshi la Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) limesema katika taarifa siku ya Jumatatu kwamba wanajeshi wake waliendelea na mashambulizi yaliyolenga maeneo ya kati na kusini mwa Gaza, likiwaua wanamgambo wenye silaha na kubomoa miundombinu yao.

Mapema siku hiyo, IDF ilidai kuwa ilikuwa imekamata wanamgambo takriban 100 kwenye operesheni katika Hospitali ya Kamal Adwan huko Jabalia kaskazini mwa Gaza.

IDF imesema operesheni hiyo ilifanywa kufuatia taarifa za kijasusi zinazoonyesha kuwa "magaidi walikuwa wameingia ndani ya hospitali," na ililenga "kuzuia shughuli za kigaidi na kuwakamata magaidi."

Wakati huo huo, mkurugenzi wa hospitali hiyo Hussam Abu Safiya, ametoa wito kwenye mtandao wa kijamii wa X kuilinda hospitali hiyo na wagonjwa na wafanyakazi wake dhidi ya mashambulizi zaidi ya Israel, akibainisha kuwa wafanyakazi 31 wa hospitali hiyo ama wamechukuliwa au kukamatwa.

Mtu akikusanya vitu kutoka kwenye kifusi baada ya shambulizi la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

Mtu akikusanya vitu kutoka kwenye kifusi baada ya shambulizi la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

Watu wakitazama nje kutoka dirishani baada ya shambulizi la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

Watu wakitazama nje kutoka dirishani baada ya shambulizi la Israeli katika kambi ya wakimbizi ya al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 28, 2024. (Picha na Marwan Dawood/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha