Katibu Mkuu wa UN atoa mwito wa kufanya juhudi za kukomesha uadui na kulinda raia wa kawaida nchini Sudan

(CRI Online) Oktoba 29, 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito wa kufanyika juhudi za kukomesha uadui na kulinda raia wa kawaida katika nchi ya Sudan inayoathiriwa na vita, akisema kuwa hivi sasa hali hairuhusu kupeleka kikosi cha Umoja huo kwa mafanikio.

Bw. Guterres amesema hayo wakati akijulisha hali ya Sudan kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja huo, akiongeza kuwa miezi 18 imepita tangu mapigano makali yaibuke kati ya Jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) huku mateso yakiongezeka siku hadi siku, na hivi sasa watu milioni 25 wanahitaji misaada.

Katika hotuba yake, Bw. Guterres amesisitiza vipaumbele vitatu katika kulinda raia wa kawaida nchini Sudan. Kwanza, pande hizo mbili zinatakiwa kukubaliana haraka kusimamisha mapigano; pili, watu wa kawaida wanatakiwa kupata ulinzi; na tatu, msaada wa kibinadamu unatakiwa kufikishwa katika sehemu hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha