UNECA yasema takwimu sahihi na za wakati ni muhimu katika kushughulikia majanga yanayoongezeka

(CRI Online) Oktoba 29, 2024

Mkurugenzi wa Kituo cha Takwimu cha Afrika kilicho chini ya Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika (UNECA) Oliver Chinganya amesema, takwimu za ubora wa juu zinazohusiana na majanga zinahitajika sana wakati Bara la Afrika na dunia kwa ujumla inakabiliwa na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi na majanga mengine.

Chinyanga amesema hayo wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Wataalamu wa Waandaaji na Watumiaji wa Takwimu Zinazohusiana na Majanga unaofanyika Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, kuanzia Oktoba 28 hadi Novemba Mosi.

Amesisitiza kuwa, katika mazingira ya sasa ambapo majanga yanayotokana na vitendo vya binadamu na ya asili yakiongezeka barani Afrika na sehemu nyingine duniani, takwimu husika zinazohusiana na majanga ni muhimu ili kuweza kuitia kwa usahihi na kushughulikia majanga yaliyopo sasa na yanayoweza kutokea katika siku za baadaye.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha