Wataalamu wakutana Kenya kujadili mikakati ya kuhimili tabianchi kwa miundombinu thabiti

(CRI Online) Oktoba 29, 2024

Wataalamu wa mabadiliko ya tabianchi wameanza mkutano wa siku nne mjini Nairobi, nchini Kenya jana Jumatatu, kujadili mikakati ya kuongeza mahitaji ya kuhimili tabianchi kwa ajili ya miundombinu thabiti.

Mkutano huo uliopewa jina la “Shule ya Waleta Mabadiliko ya Tabianchi”, na kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) na Kituo cha Kimataifa cha Kuhimili (GCA), umewaleta pamoja wataalam 50 wakati ambapo mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kutishia mifumo ya miundombinu.

Washiriki watachunguza namna ya kufanya tathmini za hatari ya tabianchi, kutambua udhaifu, na kubuni mikakati ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kuimarisha uthabiti wa miundombinu.

Mkurugenzi wa GCA kanda ya Afrika, Charles Nhemachena, amesema ulinzi wa kijamii na kiuchumi unaohusishwa na mabadiliko ya tabianchi husababisha gharama za uharibifu, ukarabati na matengenezo katika nchi nyingi.

Naye mwenyekiti wa Idara ya Sayansi za Ulimwengu na Hali ya Tabianchi katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Daniel Olago, amesema kuwa mkutano huo umeazimia kuchukua hatua kusudiwa kuziba pengo kati ya sayansi, sera, na utekelezaji wa kivitendo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha