Lugha Nyingine
Rais Xi na mwenzake wa Zambia wapongezana kwa kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa nchi zao
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Zambia Hakainde Hichilema wametumiana salamu za pongezi siku ya Jumanne kuadhimisha miaka 60 tangu nchi zao zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia.
Kwenye salamu zake, Rais Xi amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka hiyo 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya China na Zambia umestahimili majaribu ya mabadiliko katika nyanja ya kimataifa, na kila wakati pande hizo mbili zimekuwa zikidumisha urafiki wa kweli na kushikana mkono kwa ajili ya maendeleo ya pamoja.
Amesema katika miaka ya hivi karibuni, China na Zambia zimeshuhudia ziara za mara kwa mara za viongozi wa ngazi ya juu ya mara kwa mara, kuendeleza kuaminiana kisiasa, kupata manufaa kwenye ushirikiano, na zimekuwa zikiungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na masuala muhimu yanayofuatiliwa na kila upande, na kuzinufaisha nchi hizo mbili na watu wake.
Rais Xi pia amekumbusha kuwa Rais Hichilema mwezi Septemba alihudhuria Mkutano wa Kilele wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing, ambapo wawili hao kwa pamoja walitoa mwongozo wa kimkakati kwa ajili ya maendeleo ya baadaye ya uhusiano wa pande mbili.
Akibainisha kuwa anathamini maendeleo ya uhusiano kati ya China na Zambia, Rais Xi ameeleza nia yake ya kushirikiana na Rais Hichilema kuchukua maadhimisho hayo kama fursa ya kuhimiza urafiki wa jadi, kuimarisha kuungana mkono, kuimarisha ushirikiano wa pande zote, kuendeleza juhudi za ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi hizo mbili kwenye safari mpya katika zama mpya, kuimarisha uhusiano wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Zambia, na kujenga jumuiya ya karibu zaidi ya China na Zambia yenye mustakabali wa pamoja
Kwenye ujumbe wake, Rais Hichilema amesema maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia ni hatua muhimu katika uhusiano kati ya Zambia na China.
Amesema ushirika huo wa pande mbili uliojikita katika kuheshimiana, ushirikiano wenye kunufaisha pande zote na ustawi wa pamoja, umetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi hizo mbili.
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma