Rais Xi Jinping ahimiza ushirikiano zaidi kati ya China na Finland katika tasnia zinazoibukia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2024

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amefanya mazungumzo mjini Beijing na Rais wa Finland Alexander Stubb ambaye ziarani nchini China, na kusema China inaikaribisha Finland kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kupanua ushirikiano katika sekta zinazoibukia.

Ametoa wito kwa pande zote mbili kupanua ushirikiano katika mageuzi ya kijani, teknolojia ya habari, uchumi wa kidijitali, akili mnemba na nishati mpya, na kujenga muundo mpya wa ushirikiano wa kunufaishana katika zama mpya.

Rais Xi amesema Finland ni moja ya nchi za kwanza za Magharibi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China na nchi ya kwanza ya Magharibi kusaini makubaliano ya kibiashara na China.

"Wakati dunia inapitia mabadiliko ya kasi ambayo hayajawahi kuonekana katika miaka mia moja iliyopita, na hatari na changamoto zinazomkabili binadamu zinaongezeka, ushirikiano wa aina mpya wenye mtazamo wa siku za baadaye kati ya China na Finland una umuhimu wa kipekee na unapaswa kuenziwa na kuendelezwa," Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema China na Finland zinapenda amani na kutetea ushirikiano wa pande nyingi na biashara huria, akiongeza kuwa China iko tayari kuimarisha mawasiliano na ushirikiano na Finland kuhusu mabadiliko ya tabianchi, uhifadhi wa bioanuwai, maendeleo endelevu ya dunia, usimamizi wa akili mnemba na masuala mengine.

Rais Stubb amesema Finland inaheshimu na kufuata sera ya kuwepo kwa China moja na mwaka ujao iko tayari kufanya sherehe nzuri na China ya maadhimisho ya miaka 75 ya uhusiano wa kidiplomasia.

Ameongeza kuwa Finland itafanya kazi na China kuzidisha ushirikiano katika maeneo kama vile uchumi na biashara, nishati ya kijani na maendeleo endelevu.

Uchumi wa EU na China umeunganishwa, na "kutengana" au "Vita Baridi Mpya" havina maslahi ya upande wowote, Rais Stubb amesema Finland iko tayari kufanya jukumu la kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya EU na China.

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akiwa kwenye hafla ya kumkaribisha Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China na mke wake Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Finland Alexander Stubb na mke wake Suzanne Innes-Stubb kabla ya mazungumzo kati ya Marais Xi na Stubb kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China na mke wake Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Finland Alexander Stubb na mke wake Suzanne Innes-Stubb kabla ya mazungumzo kati ya Marais Xi na Stubb kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais Xi Jinping wa China akisalimiana na Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Rais Xi Jinping wa China akisalimiana na Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba Kuu la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Rais wa Finland Alexander Stubb, ambaye yuko ziarani nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha