Kampuni ya asali ya Tanzania yajipanga kupata soko kubwa la China kupitia Maonyesho ya 7 ya CIIE

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2024

Meneja uzalishaji kwa ajili ya biashara na maendeleo wa Kampuni ya Tanzania Future Enterprises, Jackson Mponela akijiandaa kufungasha asali kwenye kiwanda kilichoko Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 28, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

DAR ES SALAAM – Wafanyakazi wanne wa kampuni ya kusindika asali iliyopo Goba, mjini Dar es Salaam, Tanzania wana pilika nyingi za maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kushiriki Maonyesho ya 7 Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE), yatakayofanyika mjini Shanghai kuanzia Novemba 5 hadi Novemba 10.

Meneja uzalishaji kwa ajili ya biashara na maendeleo wa kampuni ya Tanzania Future Enterprises Bw. Jackson Mponela anasema, "Tunatarajia kuliteka soko la China la watu bilioni 1.4 kwa kuonyesha bidhaa zetu za asali wakati wa maonyesho hayo ya siku tano."

Kampuni hiyo inayozalisha, kusindika, kufungasha na kuuza bidhaa zinazotokana na ufugaji nyuki, ni miongoni mwa washiriki 34 wa Tanzania katika maonyesho hayo ya mwaka huu ya CIIE, ambapo wataonyesha bidhaa mbalimbali zikiwemo asali, mazao ya kilimo, mavazi, madini, kazi za mikono na bidhaa za viwandani.

"Bidhaa zetu za asali zitakazoonyeshwa kwenye maonyesho ya 7 ya CIIE zinajumuisha chavua ya nyuki, asali mbichi, vifuko vya asali (kwa ajili ya kukoleza utamu wa vinywaji), na nta," Mponela ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye mahojiano siku ya Jumatatu wiki hii.

Kwa kutumia kauli mbiu ya "Maskani ya Ladha Nzuri" na jina la chapa "Asali ya Jamii," Mponela ana matumaini kwamba maonyesho hayo yatafungua na kupanua soko la bidhaa za kampuni yake zinazotokana na ufugaji nyuki.

“Kampuni yetu ilianzishwa mwaka takribani mmoja uliopita, lakini uzalishaji uliongezeka Februari mwaka huu baada ya kupata mashine ya kutengeneza vifuko hivyo vya asali kutoka China, ambayo imetuwezesha kuzalisha vifuko vya asali kwa ajili ya matumizi ya majumbani na hotelini,” amesema.

Mponela amesema kampuni yake ilitambulishwa kwenye maonyesho hayo na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), shirika la serikali linalofanya kazi ya kuimarisha uchumi wa Tanzania kupitia maendeleo na utangazaji bidhaa na huduma kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Amesema anatazamia kuvutia wateja zaidi wa bidhaa zinazotokana na ufugaji nyuki katika maonyesho hayo kwa sababu, mbali na soko la China, maonyesho hayo pia yatahudhuriwa na waonyeshaji bidhaa kutoka kote duniani.

Katikati ya Oktoba, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Zanzibar nchini Tanzania Omar Said Shaaban alisema maonyesho hayo yatatoa jukwaa la kuonyesha bidhaa na huduma za Tanzania kwenye moja ya masoko makubwa zaidi ya watumiaji duniani.

“Kupitia Maonyesho hayo ya 7 ya CIIE, tunalenga kuongeza uelewa wa kimataifa kuhusu chapa ya ‘Made in Tanzania’, ambayo inaakisi ubora, uendelevu na upekee wa bidhaa zake,” alisema Shaaban. 

Meneja uzalishaji kwa ajili ya biashara na maendeleo wa Kampuni ya Tanzania Future Enterprises, Jackson Mponela akionesha bidhaa za asali kwenye kiwanda kilichoko Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 28, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

Meneja uzalishaji kwa ajili ya biashara na maendeleo wa Kampuni ya Tanzania Future Enterprises, Jackson Mponela akikagua ubora wa asali kabla ya kuifungasha ndani ya chupa kwenye kiwanda kilichoko Dar es Salaam, Tanzania, Oktoba 28, 2024. (Picha na Emmanuel Herman/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha