Lugha Nyingine
Namibia yakabidhiwa shule nne zilizojengwa kwa msaada wa China katika maeneo ya vijijini
Wanafunzi wakipata chakula kwenye bwalo la Shule ya Msingi Satotwa katika mkoa wa Kavango Magharibi nchini Namibia, Oktoba 28, 2024. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
KAVANGO MAGHARIBI, Namibia - Serikali ya Namibia Jumatatu ilikabidhiwa shule nne zilizojengwa kwa msaada wa China katika mikoa ya Kavango Magharibi na Zambezi ya nchi hiyo ambapo mradi wa ujenzi wa shule hizo, uliotekelezwa na Kundi la Kampuni za Uwekezaji wa Ujenzi la Gansu, China ulianza Machi Mwaka 2022.
Shule ya Msingi Satotwa na Shule ya Mchanganyiko ya Simanya mkoani Kavango Magharibi, pamoja na Shule za Mchanganyiko za Liselo na Masokotwani mkoani Zambezi, zote zimejengwa kwa msaada kutoka serikali ya China. Shule hizo zinajumuisha hosteli, nyumba za walimu, majengo ya utawala, madarasa, sehemu ya kunawa, maktaba na vitanda, zikinufaisha wanafunzi wapatao 1,200.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Namibia Lukas Sinimbo Muha amesema China ni rafiki wa kutegemeka wa Namibia. "Huu ni ushuhuda ambao kampuni ya China imetekeleza kufikia matarajio," amesema. "Siku za nyuma, idadi ya walimu ilikuwa ndogo kwa sababu wale ambao walilazimika kutembea umbali mrefu hawahitaji tena kufanya hivyo, kwa kuwa sasa wanaishi kwenye hosteli." ameongeza
Katika hotuba yake kwenye Shule ya Msingi Satotwa, Waziri wa Elimu, Sanaa, na Utamaduni wa Namibia Ester Anna Nghipondoka amesema kuwa mazingira bora ya kujifunzia ni muhimu kwa ajili ya kuboresha ufundishaji, kujifunza na matokeo ya kielimu. "Kwa kutoa rasilimali hizi muhimu, tunashughulikia masuala muhimu ya ufikiaji na kuwafanya wanafunzi kuwa shuleni," ameongeza.
Balozi wa China nchini Namibia Zhao Weiping amesema "shule hizo zilizojengwa kwa msaada wa China ni alama mpya za urafiki kati ya China na Namibia. Kama rafiki wa Namibia, China siku zote imekuwa na nia ya kuunga mkono maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Namibia, ikiweka kipaumbele cha elimu katika ushirikiano wetu na Namibia. "
"Ninaamini kwamba, kwa juhudi zetu za pamoja, uhusiano kati ya China na Namibia utapata maendeleo makubwa zaidi katika miaka ijayo, na kuleta manufaa zaidi halisi kwa watu wetu," ameongeza.
Mchango wa shule hizo mpya tayari umeanza kuonekana, huku idadi ya wanafunzi katika Shule ya Msingi Satotwa ikiongezeka kutoka 95 hadi 205, ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa upatikanaji wa elimu na kuimarishwa kwa ubora wa kujifunzia unaotolewa na miundombinu hiyo mipya.
Baada ya kukabidhi shule hizo nne mpya za vijijini, China sasa imetoa msaada wa shule tisa kwa Namibia tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia Mwaka 1990.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Namibia, Lukas Sinimbo Muha akihutubia kwenye hafla ya kukabidhi shule nne zilizojengwa kwa msaada wa China kwenye Shule ya Msingi Satotwa katika mkoa wa Kavango Magharibi nchini Namibia, Oktoba 28, 2024. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
Wageni wakihudhuria hafla ya kukata utepe kwenye Shule ya Msingi Satotwa katika Mkoa wa Kavango Magharibi nchini Namibia, Oktoba 28, 2024. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
Wanafunzi wakipiga picha mbele ya Shule ya Msingi Satotwa katika Mkoa wa Kavango Magharibi nchini Namibia, Oktoba 28, 2024. (Picha na Musa C Kaseke/Xinhua)
Kazi ya utafiti wa kisayansi wa fani mbalimbali yakamilika mkoani Xinjiang, China
Mandhari ya majira ya mpukutiko ya Hifadhi ya Taifa ya Ardhi Oevu ya Huaxi huko Guiyang, China
Barabara Kuu ya Jianhe-Liping yafunguliwa kwa matumizi ya umma kusini magharibi mwa China
Wanariadha wa Ethiopia washinda mbio za Marathon za Amsterdam
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma