Wataalamu na maafisa wasema ushirikiano kati ya China na Afrika unachochea ukuaji endelevu

(CRI Online) Oktoba 30, 2024

Kenya Jumanne iliandaa kongamano la 21 la mfululizo wa mihadhara ya China, ambapo washiriki wamesisitiza manufaa ya pande zote ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuendeleza maendeleo endelevu kupitia Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Naibu Mwenyekiti wa zamani wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Erastus Mwencha, amesema Afrika inaweza kupata ufahamu muhimu kutoka kwenye njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, kwa kuwa pande zote mbili zinakabiliwa na changamoto zinazofanana za maendeleo na zinaweza kufaidika na suluhu za pamoja.

Balozi wa Somalia nchini Kenya Jabril Ibrahim Abdulle amezungumzia zama mpya ya kujiimarisha na mshikamano kote barani Afrika.

Naye Zhou Yunfan wa Taasisi ya China na Afrika katika Akademia ya Sayansi ya Jamii ya China amesema ujenzi wa mambo ya kisasa ni haki ya nchi zote, pia ni kazi ya pamoja ya China na Afrika baada ya uhuru katika kutafuta maendeleo ya taifa na ustawi wa watu wao.

Likifanyika chini ya kaulimbiu ya "Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China na Ushirikiano wa kiwango cha juu wa China na Afrika chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja Njia Moja", kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Sera ya Afrika yenye makao yake makuu mjini Nairobi ikishirikiana na Taasisi ya China na Afrika na Ubalozi wa China nchini Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha