Shirika la IOM lasema watu zaidi ya milioni 14 wamepoteza makazi kutokana na mapigano nchini Sudan

(CRI Online) Oktoba 30, 2024

Shirika la Uhamiaji la Kimataifa IOM limesema, watu zaidi ya milioni 14 wamekimbia makaazi yao tangu kuzuka kwa mapigano yanayoendelea nchini Sudan.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la IOM Bi Amy Pope ametoa taarifa akisema, idadi ya wakimbizi wa ndani imefikia milioni 11, huku idadi hiyo ikiongezeka kwa laki 2 tangu mwezi wa Septemba.

Ameongeza kuwa wengine milioni 3.1 wamevuka mipaka kukimbia mapigano hayo. Kwa ujumla asilimia 30 ya watu wote wa Sudan wamekimbia makazi.

Bi Pope ameielezea hali nchini Sudan kuwa janga, huku akisema mateso yanaongezeka siku hadi siku huku watu takriban milioni 25 wakihitaji misaada.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha