

Lugha Nyingine
China yaahidi kuhimiza matumizi ya nishati mbadala wakati inapobadilisha muundo wake wa nishati kuwa wa kijani
Picha iliyopigwa Septemba 12, 2024 ikionyesha sehemu ya mtambo wa kuzalisha umeme wa megawati 50 kwa nishati ya jua kwa chumvi inayoyeyushwa katika Kitongoji cha Naomaohu cha Mji wa Hami, Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Xinhua/Hu Huhu)
BEIJING - China Jumatano imetangaza miongozo ya kuhimiza matumizi ya nishati mbadala huku kukiwa na juhudi za kupunguza matumizi ya mafuta katika kubadilisha muundo wake wa nishati kuwa wa kijani.
Miongozo hiyo, iliyotolewa na Kamati ya Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China na idara nyingine tano za serikali, inaeleza lengo la China la kutumia nishati safi badala ya nishati za kawaida.
Miongozo hiyo inabainisha kuwa matumizi ya nishati mbadala nchini China yanatarajiwa kufikia usawa wa tani zaidi ya bilioni 1.1 za makaa ya mawe ya kawaida mwaka ujao, na kuzidi usawa wa tani bilioni 1.5 za makaa ya mawe ya kawaida ifikapo Mwaka 2030.
Nchi hiyo inalenga kuongeza uwezo wake wa nishati ili kuhakikisha usambazaji salama na wa kutegemeka wa nishati mbadala, ambapo nishati mbadala zaidi itatumika katika kampuni za viwanda, usafirishaji, majengo, kilimo, maeneo ya vijijini na miundombinu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma