Maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yafanyika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2024

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema (kushoto) na Balozi wa China nchini Zambia Han Jing wakipeana mikono baada ya kuzindua bahasha ya kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wilayani Chongwe, Lusaka, Zambia. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema (kushoto) na Balozi wa China nchini Zambia Han Jing wakipeana mikono baada ya kuzindua bahasha ya kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wilayani Chongwe, Lusaka, Zambia, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

CHONGWE, Zambia - China na Zambia zimefanya hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili siku ya Jumanne, katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) wilayani Chongwe, umbali wa kilomita takriban 39 mashariki mji wa Lusaka.

Uwekaji shada la maua ulifanyika kwa heshima ya raia wa China waliofariki dunia wakati wa ujenzi wa reli hiyo ya TAZARA.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika chini ya kaulimbiu "Pitisha moyo wa TAZARA kwa kizazi kijacho na kujenga kwa pamoja mustakabali wa pamoja," yalihudhuriwa na Balozi wa China nchini Zambia Han Jing na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema vilevile na maofisa wa Ubalozi wa China na Serikali ya Zambia.

Katika hotuba yake, Balozi wa China alitoa shukrani kwa viongozi waasisi wa nchi hizo mbili kwa kuanzisha uhusiano wa kudumu ambao umeshinda majaribu ya wakati na umeonekana kuwa mfano mzuri wa uhusiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa Kusini-Kusini.

Amesema moyo usioyumba, uvumilivu, bidii na kujitolea ulioonyeshwa na watu wa China na wenyeji wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA ni hamasa na msukumo wa ushirikiano kati ya China na Zambia, na China na Afrika.

Rais wa Zambia amesema kaulimbiu hiyo ni mwafaka kwa vile inasisitiza haja ya kupitisha moyo wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa kizazi kijacho huku kukiwa na mustakabali wa pamoja.

Amesema moyo wa ushirikiano wa pamoja unadhihirika kwa jinsi nchi hizo mbili zinavyohusiana katika maeneo mbalimbali kwa miaka mingi.

Rais huyo wa Zambia amesema nchi hizo mbili zinaadhimisha miaka 60 ya ushirikiano kwa nguvu mpya na kujikita zaidi katika maana ya ushirikiano kwa serikali hizo mbili.

Pia ametoa heshima kwa raia wa China waliofariki dunia wakati wa ujenzi wa reli ya TAZARA, huku mdogo miongoni mwao alikuwa na umri wa miaka 22.

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akiweka shada la maua kuwakumbuka raia wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini, Lusaka, Zambia, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akiweka shada la maua kuwakumbuka raia wa China waliofariki wakati wa ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini, Lusaka, Zambia, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza kwenye  shughuli ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema akizungumza kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Wasanii wakitumbuiza kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia. Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

Wasanii wakitumbuiza kwenye shughuli ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Zambia yaliyofanyika katika Eneo la Kumbukumbu ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) mjini Lusaka, Zambia, Oktoba 29, 2024. (Xinhua/Peng Lijun)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha