WTO laendesha kongamano juu ya matokeo ya biashara na uchumi ya mkutano wa FOCAC wa Beijing

(CRI Online) Oktoba 31, 2024

Shirika la Biashara Duniani (WTO) limeandaa kongamano lenye kauli mbiu ya “Mtazamo wa WTO juu ya ushirikiano kati ya China na Afrika” Jumatano, tarehe 30 mjini Geneva nchini Uswisi, ambapo linafuatilia matokeo ya biashara na uchumi ya mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Kongamano hilo lilijadili matokeo muhimu yatakayopatikana kutoka kwenye mkutano huo wa FOCAC wa Beijing, kuelezea mifano ya China ya kutoa uungaji mkono kwa nchi zilizo na uchumi mdogo zaidi, na kujadili uwezekano wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuhimiza mageuzi ya WTO na kuendeleza kwa pamoja uhusiano wa ushirikiano wa kiuchumi.

Kwenye kongamano hilo, washiriki wwameeleza kuwa hatua ya hiyo ya ushirikiano wa kustawisha biashara kati ya China na Afrika itaendelea kuwa chachu kwenye ushirikiano wa pande hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha