Sudan Kusini na IOM zazindua mpango wa kuunga mkono juhudi za kutafuta suluhu kwa watu waliokimbia makazi yao

(CRI Online) Oktoba 31, 2024

Sudan Kusini ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), zimezindua mpango wa kutafuta suluhu kwa watu waliokimbia makazi yao siku ya Jumatano unaolenga kuwezesha wadau wa masuala ya kibinadamu na maendeleo kutojikita kwenye juhudi za kukabiliana na dharura pekee na badala yake kutekeleza programu ya mpito na ya uokoaji.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango huo mjini Juba, mkuu wa Shirika la IOM nchini Sudan Kusini Vijaya Souri amesema mpango huo utawezesha juhudi za pamoja na washirika wao kutoa suluhu kwa watu waliokimbia makazi yao na pia kuweka mipango yenye kutoa suluhu ya muda mrefu kwa jamii kuhimili athari za siku zijazo.

Amebainisha kuwa ni muhimu kwao kuwa na uwezo wa kufanya kazi na washirika, kuweza kuachana na kujikita pekee na mwitikio wa kibinadamu na badala yake kujikita zaidi katika suluhu za mpito na uokoaji, uhamishaji na kuweza kusuka mipango inayowapa wanajamii suluhu za muda mrefu ili kuwa na maisha mazuri.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha