Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping asaini amri ya kutangaza kwa umma kanuni za kuimarisha usimamizi wa askari wa akiba
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), amesaini amri ya kutangaza kwa umma kanuni za kipindi cha mpito, zikiwa na lengo la kuwezesha utekelezaji wa sheria za usimamizi wa askari wa akiba.
Kanuni hizo zinajikita katika kuweka muundo wa usimamizi wa askari wa akiba katika zama mpya, zikifafanua kwa kina michakato ya uteuzi, upandishaji vyeo, kupangiwa majukumu, mafunzo, tathmini, marupurupu na kustaafu.
Kutangazwa kwa umma kwa kanuni hizo ni matokeo muhimu ya mageuzi ya kijeshi ya China ya rasilimali watu, na kunaashiria hatua muhimu katika kuboresha usimamizi wa kisheria, kivigezo na kisayansi wa askari wa akiba, na kuhimiza uwezo wa hali ya juu na wa kiweledi wa jeshi la akiba la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma