Mgogoro wa kijeshi nchini Sudan wasababisha vifo vya wanahabari 14

(CRI Online) Novemba 04, 2024

Shirikisho la waandishi wa habari la Sudan hivi karibuni limesema, wanahabari 13 nchini humo wameuawa, wakiwemo wanahabari wawili wanawake, tangu mwezi Aprili mwaka jana mapigano kati ya jeshi la Sudan na jeshi la RSF yalipoanza.

Katika taarifa yake, Shirikisho hilo limesema, mapigano hayo yanayoendelea yamesababisha wanahabari 186 kushambuliwa, kuzuiliwa, kuibiwa na kutishiwa maisha, huku mamia ya wanahabari wakilazimishwa kukimbia makazi yao, hivyo kuwa na athari mbaya katika sekta ya habari nchini humo.

Shirikisho hilo limezitaka pande mbalimbali ziwalinde wanahabari, na kutoa masharti muhimu kwa ajili ya kushughulikia kazi za sekta ya habari.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha