Mawaziri wa Afrika wataka kuanzisha benki ya kikanda ya nishati

(CRI Online) Novemba 04, 2024

Mawaziri wa nishati kutoka nchi 18 za Afrika wamekutana nchini Cameroon kujadili uwezekano wa kuanzisha benki ya kuongeza uzalishaji wa nishati.

Mawaziri hao waliokutana chini ya ufadhili wa Shirika la Wazalishaji wa Petroli la Afrika (APPO), walionesha matarajio ya kuanzisha Benki ya Nishati ya Afrika (AEB).

Katika hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Cameroon Joseph Dion Ngute amepongeza uamuzi wa Baraza la Mawaziri wa kutafiti uwezekano wa kuanzisha benki hiyo, na kuongeza kuwa, ingawa kazi zaidi bado inahitajika kufanywa kabla ya benki hiyo kuanza shughuli zake, ni dhahiri kuwa itakuwa msukumo wa kukamilisha miradi ya mafuta barani Afrika.

Ameongeza kuwa, AEB ambao ni mpango wa pamoja wa APPO na Benki ya Uagizaji na Uingizaji ya Afrika, itaweza kushughulikia vikwazo vya kifedha katika sekta za mafuta na gesi, na kupunguza mzigo wa mageuzi ya nishati barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha