Tanzania yazindua kituo cha mafunzo ya ukunga ili kupunguza vifo vya watoto wachanga

(CRI Online) Novemba 04, 2024

Tanzania imezindua Kituo cha Ukunga cha Malaika wa Maisha, cha kwanza cha aina yake nchini humo kwa lengo la kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga.

Hafla ya uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam, iliandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Kuboresha Urafiki kati ya Tanzania na China na Chuo Kikuu cha Tiba cha Wenzhou cha nchini China.

Akizungumza katika hafla hiyo, katibu mkuu wa Shirikisho hilo Joseph Kahama ameishukuru China kwa kuanzisha kituo hicho, akisema kitatoa mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Ofisa mkuu mwandamizi na mratibu wa Mradi wa Ukunga wa Malaika wa Uhai barani Afrika Dong Qixin amesema, madaktari wa China watatoa mafunzo kwa wakunga nchini Tanzania, huku wakunga kati ya 20 hadi 30 wakifundikwa katika kila awamu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania, kiwango cha vifo vya watoto wachanga nchini humo kwa mwaka huu kinatarajiwa kuwa 33.021 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa hai, ikiwa ni pungufu kutoka asilimia 3.36 ya mwaka jana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha