Semina ya kwanza ya kuboresha mafunzo ya lugha ya Kichina yafanyika nchini Ethiopia

(CRI Online) Novemba 04, 2024

Semina ya kwanza ya mwaka kuhusu mafunzo ya lugha ya Kichina imefanyika ijumaa iliyopita mjini Addis Ababa, Ethiopia, na kusisitiza haja ya kuboresha mafunzo ya lugha ya Kichina nchini humo.

Hafla hiyo iliyowakutanisha wakufunzi na wataalamu wa lugha kutoka China na Ethiopia, ililenga kuanzisha mfumo wa ufanisi wa mafunzo ya lugha ya Kichina nchini Ethiopia na kukabliana na changamoto zinazotokana na mchakato huo.

Akizungumza katika semina hiyo, naibu mkuu wa Mamlaka ya Elimu mkoani Oromia, Bultosa Hirko amesema lugha ya Kichina inaendelea kupata umaarufu nchini Ethiopia, na kutoa fursa za kiuchumi, kuboresha mawasiliano ya kitamaduni, na kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

Naye konsela wa mambo ya utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Ethiopia, Zhang Yawei amesema, semina hiyo inalenga kubadilishana uzoefu, kuendeleza mafanikio, kukabiliana na changamoto na kwa pamoja kuendeleza mafunzo ya lugha ya Kichina nchini Ethiopia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha