

Lugha Nyingine
Mtaalamu wa Kenya asema biashara na China imeboresha ustawi wa maisha ya Waafrika
Biashara inayoshamiri kati ya nchi za Afrika na China imesaidia katika upatikanaji wa nafasi za ajira na kuinua kiwango cha maisha katika nchi za Afrika.
Hayo yamesemwa na mchumi wa Kenya Profesa Xn Iraki wa Chuo Kikuu cha Nairobi cha Kenya alipohojiwa na Shirika la Habari la China, Xinhua. Profesa Iraki amesisitiza nafasi muhimu ya usawa wa kibiashara kama msingi wa kunufaishana, na kuchochea maendeleo ya kasi barani Afrika na China.
Profesa Iraki pia amesisitiza umuhimu wa majukwaa ya majadiliano kati ya China na nchi za Afrika, kama vile Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), ambayo yanachukua nafasi muhimu kama njia ya kutimiza maslahi ya pamoja, kukabiliana na changamoto za kibiashara, na kutumia fursa ambazo bado hazijatumika.
Pia amependekeza uhusiano wa uwazi kati ya wafanyabiashara wa pande hizo mbili na kutafiti maeneo mapya ya kibiashara bila kujali umbali wa kijiografia kati ya China na nchi za Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma