

Lugha Nyingine
Benki ya Dunia yakubali kutenga dola za Marekani milioni 354 kusaidia Sudan
Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Sudan Bw. Jibril Ibrahim amesema Benki ya Dunia imekubali kutenga dola za Marekani milioni 354 kusaidia Sudan kutekeleza miradi mingi ya dharura.
Bw. Ibrahim amesema, fedha hizo zitatolewa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayoshirikiana na serikali ya Sudan ifikapo Juni mwaka 2025. Kati ya fedha hizo, dola milioni 130 zitatumika kwa ajili ya usambazaji wa chakula, dola milioni 100 zitatumika kukabiliana na dharura za kijamii, dola milioni 82 zitatumika kupunguza majanga ya kiafya, na dola milioni 42 zitatumika kwa mipango ya dharura ya elimu.
Bw. Ibrahim pia amesema, mapigano yanayoendelea nchini Sudan yamesababisha hasara ya kiuchumi ambayo ni vigumu kukadiria, na kutoa wito kwa wafadhili wote kutimiza ahadi zao ili kukidhi mahitaji ya haraka ya Sudan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma