

Lugha Nyingine
Mauzo ya nje ya Kenya kwa nchi za Afrika yaripotiwa kuongezeka
Ripoti ya kiuchumi iliyotolewa jana jumatatu na Benki Kuu ya Kenya imeonyesha kuwa, mauzo ya Kenya kwa nchi nyingine za Afrika, yakichochewa na kuongezeka kwa usafirishaji na kuimarishwa kwa uhusiano wa pande mbili, yameongezeka kwa asilimia 26 katika miezi saba ya kwanza ya mwaka 2024.
Benki hiyo imesema mauzo ya nje ya Kenya yaliongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 248.7, sawa na dola za kimarekani bilioni 1.93, ikiongezeka kutoka dola bilioni 1.53 katika kipindi kama hicho mwaka 2023.
Kwa mujibu wa benki hiyo, sehemu kubwa ya mauzo ya nje kutoka Kenya yaliuzwa katika nchi za Uganda, Tanzania na Rwanda pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Afrika Kusini ambazo zina mahitaji makubwa.
Mauzo ya nje ya nchi hiyo yanahusisha zaidi chai, kahawa, wanyama, mafuta ya mbogamboga, mabaki ya mkaa, unga wa ngano na bidhaa za viwandani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma