Mradi wa Mianzi wa China waboresha mazingira ya maeneo ya Kenya yaliyoathiriwa na mafuriko ya maji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 05, 2024

Mtu akionesha mianzi inayopandwa kando ya Mto Kirinyaga kwenye Kaunti ya Kirinyaga, Kenya, Agosti 26, 2024. (Picha na Robert Manyara/Xinhua)

Mtu akionesha mianzi inayopandwa kando ya Mto Kirinyaga kwenye Kaunti ya Kirinyaga, Kenya, Agosti 26, 2024. (Picha na Robert Manyara/Xinhua)

Katika miongo mingi iliyopita, shamba la Francis Mayobo lililopo kando ya Mto Nzoia Magharibi mwa Kenya limekumbwa na mafuriko ya maji mara kwa mara, ambayo yaliharibu nafaka zake na kumfanya akaribie kufilisika.

Mayobo akiwa ofisa wa miradi ya kiumma aliyestaafu, ana shamba lililopo karibu na mto, ambao chanzo chake kipo kwenye nyanda za juu za Kaskazini Magharibi mwa Kenya na unatiririka mpaka kwenye Ziwa Viktoria.

Miaka minne iliyopita, Mayobo alipanda mamia ya mianzi kwenye shamba lake baada ya kujua uwezo wa mianzi katika kuzuia mafuriko ya maji.

“Nilihamasishwa kupanda mianzi baada ya mafunzo na utafiti kuhusu namna mianzi inavyoweza kulinda shamba langu kutoka mafuriko ya maji,” Mayobo aliliambia shirika la habari la China Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Kwa sasa mianzi siyo tu inalinda shamba lake kutoka mafuriko ya maji, bali pia imerudisha uhai wa ardhi na kumwezesha kulima mazao kama vile mahindi, maharage, ndizi na mtama.

Mayobo ni mmoja kati ya wakulima wenye mashamba madogo katika eneo la Magharibi mwa Kenya lililoathiriwa mara kwa mara na mafuriko ya maji, ambao wananufaika na mradi wa mianzi uliofadhiliwa na Akademia ya Sayansi ya China kwa kupitia kituo chake cha Utafiti wa Pamoja cha China na Afrika.

Mradi huo unatekelezwa na shirika la ushirikiano wa kimataifa wa usimamizi wa mfumo wa mazingira ya asili chini ya Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (UNEP-IEMP), pamoja na washirika wake wenyeji.

Mradi huo unaoitwa “Urejeshaji wa Mazingira ya Asili ili Kuboresha Maisha na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi: Ushirikiano kati ya China na Kenya kwenye Teknolojia ya Mianzi,” unaahidi kuzuia mafuriko ya maji, kuongeza mapato na kuimarisha uhimilivu wa wakulima na wavuvi wenyeji.

Chini ya mradi huo, Mayobo na wakulima wengine wamepokea mafunzo kuhusu upandaji mianzi yanayowasaidia kujenga mashamba na kuhifadhi miche kwa kupandwa tena katika maeneo yanayoathiriwa mara kwa mara na mafuriko.

Edmond Machoki akiwa kwenye kibanda chake pamoja na bidhaa za mianzi kwenye maonesho katika Kaunti ya Nyeri, katikati mwa Kenya, Septemba 13, 2024. (Pich na Robert Manyara/Xinhua)

Edmond Machoki akiwa kwenye kibanda chake pamoja na bidhaa za mianzi kwenye maonesho katika Kaunti ya Nyeri, katikati mwa Kenya, Septemba 13, 2024. (Pich na Robert Manyara/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha