WHO yatoa wito wa upatikanaji endelevu wa maji safi na usafi ili kudhibiti milipuko ya kipindupindu nchini Somalia

(CRI Online) Novemba 05, 2024

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa wadau nchini Somalia kutoa kipaumbele katika upatikanaji wa maji safi, kuboresha usafi, na kusaidia usambazaji wa chanjo ya kipindupindu ili kusaidia kukabiliana na milipuko inayojirudia ya ugonjwa huo.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu, WHO imesema kipindupindu bado ni changamoto kubwa ya kiafya nchini Somalia, hususan katika mikoa iliyoathiriwa na mapigano na wakimbizi wa ndani, na maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji safi na ambayo yanakabiliwa na changamoto ya usafi.

Kwa mujibu wa Shirika hilo, Somalia imerekodi kesi mpya 768 za kipindupindu katika wiki nne zilizopita kwenye wilaya 31, huku kesi zikiongezeka katika maeneo ya Kismayu, Jowhar, Marka, Burhakab, Barawe, Borama na Baidoa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha