Tanzania yashuhudia ongezeko la watalii kutoka China

(CRI Online) Novemba 05, 2024

Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Hassan Abbasi, amesema idadi ya watalii wa China wanaotembelea vivutio vya utalii nchini Tanzania imeongezeka kidhahiri tangu kumalizika kwa janga la COVID-19.

Bw. Abbasi amesema, watalii 54,444 kutoka China wametembelea Tanzania kati ya mwezi Januari na Septemba mwaka huu, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya ile iliyorekodiwa mwaka jana.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam kabla ya tukio la Ushirikiano wa Tanzania na China katika Utalii na Utamaduni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 ya uhusiano imara wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Amesema mwaka 2018, kabla ya mlipuko wa COVID-19, watalii 32,000 walitembelea Tanzania, idadi ambayo iliongezeka na kufikia 44,038 mwaka 2023.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha