Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Botswana

(CRI Online) Novemba 06, 2024

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Botswana, Duma Boko kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya uhusiano kati ya nchi mbili China na Botswana yamedumisha mwelekeo mzuri, na pande hizo mbili zimepata matokeo mazuri katika ushirikiano kwenye sekta za miundombinu, nishati safi, na matibabu na afya.

Rais Xi amesisitiza kuwa, anaweka mkazo mkubwa katika maendeleo ya uhusiano kati ya pande hizo mbili, na anapenda kufanya juhudi pamoja na rais mteule Boko katika kuhimiza ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili hadi kwenye kiwango cha juu zaidi, ili kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha