Lugha Nyingine
Ziwa Qinghai larejea kwenye hali nzuri kutokana na ongezeko la mvua na uhifadhi wa mazingira
Watalii wakitembelea kivutio cha utalii cha Ziwa Qinghai Mkoani Qinghai, China, Oktoba 18, 2024. (Xinhua/Zhang Long)
Ziwa Qinghai, ziwa kubwa zaidi la chumvi nchini China lisilounganishwa na bahari, limeendelea kupanuka katika miaka 20 iliyopita, huku kiwango chake cha maji kikiinua kwa wastani wa sentimita 20 kila mwaka.
Mwishoni mwa Septemba mwaka huu satilaiti ya kuhisi kwa mbali iligundua kuwa, ukubwa wa ziwa hilo umefikia zaidi ya kilomita za mraba 4,650, ambao umerejea kwenye ukubwa wake wa miaka 70 iliyopita.
Ziwa Qinghai lililopo Kaskazini Magharibi mwa Nyanda za Juu za Qinghai-Xizang ni kizuizi muhimu cha kiikolojia Kaskazini mwa China, na pia ni sehemu muhimu ya kupumzika kwa ndege wanaohama.
Sun Jianqing, ofisa wa Shirika la Usimamizi wa Hifadhi ya Kitaifa ya Mazingira ya Asili ya Ziwa Qinghai alisema, kurejea kwa ukubwa wa Ziwa Qinghai kunatokana na sababu nyingi zikiweko mvua nyingi zaidi kwenye Kaskazini Magharibi mwa China, hatua zenye mafanikio katika kuhifadhi maingira, na juhudi za kurejesha hali ya ziwa hilo katika miaka 20 iliyopita.
Picha iliyopigwa Oktoba 18, 2024 ikionesha kivutio cha utalii cha Ziwa Qinghai mkoani Qinghai, China. (Xinhua/Zhang Long)

people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma