

Lugha Nyingine
Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC Li Xi afanya ziara nchini Kenya
Tarehe 4, Novemba kwa saa za huko Nairobi, Li Xi akikutana na rais William Ruto wa Kenya. (Picha na Li Xiang/Xinhua)
Mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Bw. Li Xi amefanya ziara nchini Kenya kuanzia tarehe 3 hadi tarehe 5 Novemba, ambapo amekutana na rais William Ruto wa Kenya.
Bw. Li Xi amesema China inapenda kushirikiana na Kenya kuwa marafiki na wenzi wa kuaminiana, kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya kila upande na yanayofuatiliwa na kila upande, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya karibu zaidi ya China na Kenya yenye mustakbali wa pamoja katika zama mpya. Amesema, rais Xi Jinping wa China alitangaza hatua 10 za kuhimiza juhudi za kuelekea kuwa nchi za mambo ya kisasa kupitia ushirikiano kati ya China na Afrika katika mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC wa mwaka 2024, China inapenda kuunganisha matokeo ya mkutano huo na ruwaza ya mwaka 2030 ya Kenya, ili kusaidia maendeleo ya uchumi wa Kenya.
Bw. Li Xi ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na Kenya katika kuimarisha mawasiliano na uratibu kwenye masuala kama vile mageuzi ya mashirika ya kimataifa ya pande nyingi, na kushirikiana kulinda maslahi ya pamoja ya nchi za Kusini.
Kwa upande wake Rais Ruto amesema, Kenya inaunga mkono hatua 10 zilizotolewa na rais Xi katika mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC wa mwaka 2024, na itashirikiana na China kuhimiza utekelezaji wa matokeo ya mkutano huo. Amesema Kenya inapenda kuimarisha mawasiliano na China, kuhimiza ushirikiano na mshikamano kati ya nchi za Kusini, na kuitarajia China ishiriki zaidi katika mambo ya Afrika na ujenzi wa Umoja wa Afrika, na kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma