Ushirikiano wa hali ya juu kati ya China na Afrika waongoza katika kutimiza mambo ya kisasa kwa nchi za Dunia ya Kusini

(CRI Online) Novemba 06, 2024

Mkutano wa Baraza la "Maendeleo Endelevu ya Dunia ya Kusini na Ushirikiano kati ya China na Afrika" umefanyika jana huko Hongqiao, China katika wakati wa kufanyika kwa Mkutano wa 7 wa Baraza la Kimataifa la Uchumi.

Naibu Waziri wa Biashara wa China Bw. Li Fei alisema kuwa, China ni mwanachama wa Dunia ya Kusini na daima imekuwa ikiunga mkono kwa vitendo maendeleo endelevu ya nchi zilizo kwenye kanda hiyo. Amesema China inapenda kushirikiana na nchi za Dunia ya Kusini katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa kivitendo, kubadilishana uzoefu wa maendeleo ya mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China, na kutekeleza kwa pamoja Ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda Bw. Prudence Sebahizi amesema, kutokana na ujenzi wa pamoja wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na mapendekezo matatu makuu kwa dunia yaliyotolewa na China, idadi kubwa ya nchi zinazoendelea pamoja na Rwanda zimepata manufaa halisi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha