

Lugha Nyingine
Mradi ya mafunzo ya China yaisaidia Zanzibar kuboresha matibabu kwa watoto
China Jumanne ilizindua awamu mpya wa mradi wa mafunzo katika Zanzibar nchini Tanzania ili kuboresha uwezo wake wa matibabu kwa watoto na kupunguza kiwango cha vifo vya watoto.
Mafunzo ya mwaka huu yaliyoandaliwa na Wizara ya Biashara ya China na kutekelezwa na Hospitali ya Watoto ya Hunan, yalianza katika hospitali ya wilaya ya Lumumba Unguja, wanafunzi 50 kutoka kisiwa cha Unguja na Pemba walihudhuria Hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo ya mwezi mzima. Wote walikuwa wafanyakazi wa matibabu ya watoto katika hospitali huko, ikiwa ni pamoja na madaktari wa watoto, madaktari wa upasuaji, madaktari wa ganzi na wauguzi wa watoto.
“Kuboresha huduma ya matibabu kwa watoto na kulinda afya za watoto ni majukumu na dhamira zetu sote,” alisema Zhang Ming, Kaimu Balozi Mdogo wa China kisiwani Zanzibar, alihutubia hafla hiyo akisema.
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya Watoto ya Hunan Qu Shuangquan alisema kwamba hospitali hiyo ikitilia maanani sana mradi huu wa mafunzo, wamefanya mikutano kadhaa maalum ya kupitia mpango wa utekelezaji wa mradi huo, na wamechagua wataalam wa matibabu kwa watoto, kutekeleza kazi za mafunzo.
Naibu Waziri wa Afya wa Zanzibar Hassan Khamis Hafidh alishukuru sana kwa msaada wa China, akitarajia ushirikiano zaidi kati ya China na Zanzibar katika masuala ya matibabu kwa watoto. Pia amewataka madaktari na wauguzi kuchangamkia fursa ya mafunzo hayo kwa kujifunza kwa bidii.
Hospitali ya watoto ya Hunan imetuma vikundi vya wataalam visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa mafunzo ya matibabu kwa watoto tangu mwaka 2017 na imetoa mafunzo kwa wataalam 120 wa matibabu wa Zanzibar.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma