Rais wa China asisitiza kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu ya kazi za jamii

(CRI Online) Novemba 07, 2024

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alitoa maagizo muhimu kuhusu kazi za jamii, akisema kazi hizo ni sehemu muhimu ya kazi za Chama cha Kikomunisti cha China na nchi , na zinahusisha utawala wa muda mrefu wa Chama, amani ya muda mrefu ya nchi, utulivu na uwiano wa jamii, na maisha ya furaha ya wananchi.

Rais Xi amesema, ni lazima kuimarisha ushawishi wa Chama katika sekta mpya zinazoibuka, kuimarisha uongozi wa Chama katika usimamizi wa ngazi ya shina, na kuhudumia vizuri wananchi ili kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu ya kazi za jamii katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha