Trump ashinda uchaguzi wa rais nchini Marekani

(CRI Online) Novemba 07, 2024

Vyombo vingi vya habari nchini Marekani vimetabiri kuwa mgombea urais kutoka chama cha Republican, Donald Trump, amepata kura za kutosha za wajumbe wa kamati maalum ya uchaguzi na kushinda uchaguzi huo, na hivyo kuibua wasiwasi wa umma.

Katika uchaguzi wa rais nchini Marekani, mgombea aliyepata kura zaidi ya nusu za wajumbe wa kamati hiyo maalum yenye watu 538 anakuwa mshindi wa uchaguzi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amempongeza Trump kwa ushindi huo kupitia mtandao wa kijamii wa X, akisema yuko tayari kufanya juhudi pamoja na Trump kwa ajili ya amani na ustawi zaidi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kupitia mtandao wa X imesema, Waziri Mkuu huyo amempongeza Trump kwa ushindi huo na kusema ni mwanzo mpya kwa taifa la Marekani, na kusema huo ni ushindi kwa mataifa hayo mawili.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha