Lugha Nyingine
Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa rais mteule wa Marekani
Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi ametuma salamu za pongezi kwa Bw. Donald Trump kwa kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Marekani.
Rais Xi ameeleza kuwa, historia imethibitisha kuwa ushirikiano kati ya China na Marekani unazinufaisha pande zote mbili, na mapambano kati ya nchi hizo yana athari mbaya. Amesema uhusiano wenye utulivu, hali nzuri na maendeleo endelevu kati ya China na Marekani unaendana na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili na matarajio ya jumuiya ya kimataifa.
Rais Xi amesema anatumaini kuwa pande zote mbili zitashikilia kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha mazungumzo na mawasiliano, kushughulikia ipasavyo tofauti, na kutafuta njia mwafaka kwa nchi hizo mbili kutendeana kwa usahihi katika kipindi kipya, ili kunufaisha pande zote mbili na dunia nzima.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma