Waziri wa Biashara wa Rwanda asema CIIE ni maalum kwa aina yake, fursa na China kufungua soko kwa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2024

Picha iliyopigwa kwenye skrini ikimuonyesha Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi akiwa kwenye mahojiano maalum na People’s Daily Online.

Picha iliyopigwa kwenye skrini ikimuonyesha Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi akiwa kwenye mahojiano maalum na People’s Daily Online.

Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi amesema Maonyesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) ni maalum kwa aina yake kwa kuwa ni pekee yenye kujikita katika uagizaji bidhaa kutoka nje hivyo kuwa jukwaa la China kufungua soko lake na kutoa fursa kwa ulimwengu wa nje.

Sebahizi ameyasema hayo Jumatano, Novemba 6 kwenye mahojiano maalum na People’s Daily Online yaliyofanyika kwenye banda la Rwanda la maonyesho ya 7 ya CIIE yanayoendelea mjini Shanghai, Mashariki mwa China ambapo Rwanda ni moja ya nchi za Afrika zinazoshiriki kwenye maonyesho hayo.

“Kwanza, hii CIIE ni maalum kwa aina yake, na kwakuwa ni dhahiri kwamba ni maonyesho pekee ambayo huvutia bidhaa za kuagizwa kutoka nje, ni jambo la kuvutia sana. Hivyo, China inafungua soko lake yenyewe kwa ulimwengu wa nje” amesema Sebahizi, akiongeza kuwa, hili la China kufungua soko lake halidhihirishwi tu na maonyesho hayo ya CIIE bali na ukweli kwamba, China pia imeondoa ushuru unaotozwa kwenye bidhaa kutoka nchi zenye uchumi mdogo zinazoingia kwenye soko lake.

Pili, Sebahizi amesema kuwa, kwa kuwa na maonyesho hayo ya CIIE kunatoa fursa kwa kampuni za Rwanda na nchi za Afrika kwa ujumla wake, kujenga mitandao ya kibiashara, kuzipa fursa ya kujifunza na kuchangia uzoefu, kuanzisha mawasiliano na pia kusaidia kampuni za China kuona fursa ambamo zinaweza kuwekeza zitakapokwenda Afrika.

“Kwahiyo kuna makubaliano ya kibiashara, kunakuchangia uzoefu, kunakujifunza kutoka kwa kila mmoja, na pia ufikiaji wa masoko na fursa kwa pande zote zinazoshiriki” amesema.

Amebainisha kuwa, kwenye maonyesho ya mwaka huu, Rwanda ina kampuni tano zinazoonesha bidhaa mbalimbali zikiwemo za kahawa, asali iliyosindikwa, pilipili, mafuta ya kupikia, bidhaa za kijadi za kazi za mikono, kunadi uwekezaji na chapa ya “Visit Rwanda” sambamba na uwepo wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) inayoonesha fursa mbalimbali zinazopatikana Rwanda.

Ameeleza kuwa tangu Rwanda ianze juhudi za kuingia kwenye soko la biashara ya mtandaoni la China kupitia kampeni ya kunadi bidhaa zake moja kwa moja mtandaoni kwa wanunuzi Wachina, imekuwa ikishuhudia kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa zake kama vile pilipili, kahawa na asali kiasi kwamba changamoto kubwa imebaki kwenye uwezo wa uzalishaji wa Rwanda ili kukidhi soko la China.

“Tumeshuhudia idadi ya mahitaji ikiongezeka muda hadi muda…mathalan, mahitaji ya pilipili yameongezeka kwenda juu kwa miaka kadhaa kiasi kwamba changamoto tuliyonayo sasa Rwanda ni kuongeza uwezo wa uzalishaji” amesema.

Picha ikimuonyesha Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi akiwa na timu ya waandishi wa habari wa People’s Daily Online kwenye banda la Rwanda baada ya mahojiano. (Picha kwa hisani ya Timu ya Mawasiliano ya Rwanda)

Picha ikimuonyesha Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Prudence Sebahizi akiionesha timu ya waandishi wa habari wa People’s Daily Online banda la Rwanda baada ya mahojiano. (Picha kwa hisani ya Timu ya Mawasiliano ya Rwanda)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha