Bidhaa nyingi zaidi kutoka nchi zilizo nyuma kiuchumi zaingia kwenye soko la China

(CRI Online) Novemba 08, 2024

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning jana amesema, kuanzia Maoneshao ya kwanza ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa(CIIE) kufanyika nchini China, nchi nyingi zilizo nyuma kiuchumi zimepata fursa ya kushiriki maoneshao hayo kwa urahisi.

Amesema katika miaka saba iliyopita tangu kuanzishwa kwa maonyesho hayo, bidhaa nyingi zaidi kutoka nchi zilizo nyuma kiuchumi zimeingia kwenye soko la China, na kuhimiza maendeleo ya sekta husika katika nchi hizo, na pia kuboresha maisha ya wananchi wao.

Bi. Mao pia amesema, kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, China itaagiza bidhaa kutoka nchi zilizo nyuma kiuchumi bila ya kuzitoza ushuru.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha