Wajenzi wa Barabara wa China nchini Uganda wasifiwa kwa kushiriki kwenye mambo ya jamii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 08, 2024

Tarehe 28, Oktoba, wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba wakitembelea  eneo la kuchimba mawe karibu na kambi ya ujenzi wa barabara ya  China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Wakati Chuo cha Teknolojia cha Buhimba na Kampuni ya Kundi la Saba la Reli ya China (CRSG) zilipotia saini kwenye makubaliano ya maelewano ya ushirikiano (MoU), mwanafunzi wa kozi ya Uhandisi wa Ujenzi Peninah Nasambu mwenye umri wa 20 pamoja na makumi ya wanafunzi wenzake walitembelea maaraba, eneo la kuchimba mawe na ghala kwenye kambi hiyo. Safari hii imewawezesha vijana hao kujionea jinsi barabara linavyojengwa kuanzia mwanzo kabisa.

Wilaya ya Kikuube ni moja kati ya maeneo yenye maliasili nyingi zaidi za mafuta ghafi, eneo hilo bado halijahuishwa zaidi kwa sababu ya kuwa mbali na miji. Hivi sasa, chini ya uungaji mkono wa washirika likiwemo kundi la CRSG, serikali ya Uganda inajenga “barabara ya mafuta” la kuunganishwa vizuri na eneo hilo ili kuhimiza maendeleo ya viwanda vya maliasili.

Uhusiano wa ushirikiano huo pia umenufaisha wanafunzi wa Nasambu, ukiwapa fursa za kupata mafunzo, kufanya mazoezi, na kutarajia kupata nafasi za ajira.

Tarehe 28, Oktoba, wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba wakitembelea eneo la kuchimba mawe karibu na kambi ya ujenzi wa barabara ya China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 28, Oktoba, wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba wakitembelea eneo la kuchimba mawe karibu na kambi ya ujenzi wa barabara ya China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Mwakilishi wa kundi la CRSG nchini Uganda Chen Hai alisema, “ Tunajikita katika kazi zetu hapa za kuhimiza elimu ya hapa na kuongeza nafasi za ajira za wenyeji hapa.”

Charles Piido, mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba alisema, zaidi ya asilimia 80 ya waajiriwa wa kundi la CRSG wanatoka maeneo ya karibu , hali ambayo imeongeza mawasiliano kati ya kampuni hiyo na jamii ya wakazi.

Katumba Wamala, Waziri wa Uhandisi na Mawasiliano wa Uganda alishiriki kwenye hafla ya utiaji saini wa Makubaliano ya Maelewano ya Ushirikiano, ambapo alisifu sana kundi la CRSG kupenda kunufaika pamoja na watu wa Uganda na ujuzi wa ufundi. Alisisitiza kuwa, ushirikiano huo umeunga mkono lengo la serikali la kutoa mafunzo ya kazi za ufundi kwa vijana, ili waweze kupata kazi endelevu.

Tarehe 28, Oktoba, Chen Hai, mwakilishi wa kundi la CRSG nchini Uganda akihojiwa na Shirika la Habari la China Xinhua karibu na kambi ya ujenzi wa barabara ya China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 28, Oktoba, wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba wakitembelea  ghala ya kambi ya ujenzi wa barabara ya China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

Tarehe 28, Oktoba, wanafunzi wa Chuo cha Teknolojia cha Buhimba wakitembelea ghala ya kambi ya ujenzi wa barabara ya China huko Kikuube, Magharibi mwa Uganda. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha