China na Umoja wa Afrika zaahidi kuimarisha ushirikiano wa kimkakati chini ya mfumo wa FOCAC

(CRI Online) Novemba 08, 2024

China na Umoja wa Afrika (AU) zimeahidi kuimarisha zaidi ushirikiano wao wa kimkakati chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Ahadi hiyo imetolewa jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wakati wa semina ambapo maofisa na wataalam wa China na Umoja wa Afrika walijadili kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya kwenye mazingira yote.

Ofisa Mkuu wa Kamati ya Uchumi, Jamii na Utamaduni ya Umoja wa Afrika Khalid Boudai amesema, uhusiano wa China na Afrika unatoa fursa ya kuiga masuala ya kiutawala ambayo yanawezesha watu wa Afrika na taasisi pia.

Mkuu wa ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Hu Changchun amesema, China na Afrika zinatakiwa kuimarisha zaidi ushirikiano wao, na kulenga kuboresha ustawi wa watu wa China na Afrika na kudumisha amani na utulivu wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha