Watu 7 wauawa katika shambulizi la anga la Israel karibu na Damascus nchini Syria

(CRI Online) Novemba 11, 2024

Wizara ya ulinzi ya Syria imeripoti kuwa raia saba, wakiwemo wanawake na watoto, wameuawa na wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulizi la anga la Israel lililofanywa jana jioni karibu na mji wa Damascus.

Wizara hiyo imesema katika taarifa yake kuwa karibu saa 11 asubuhi, Israel ilifanya shambulizi la anga kutoka eneo la Milima ya Golan linalokaliwa, likilenga jengo la makazi katika eneo la Sayyidah Zaynab katika kitongoji cha Damascus. Shambulizi hilo pia limesababisha hasara kubwa kwa mali binafsi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha