Misri na Malaysia zahimiza amani na usalama katika Mashariki ya Kati

(CRI Online) Novemba 11, 2024

Misri na Malaysia zimetoa mwito kutimiza amani na usalama katika eneo la Mashariki ya Kati.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Misri, mwito huo umetolewa katika taarifa ya pamoja kufuatia mkutano uliofanyika kati ya Rais Abdel-Fattah al-Sisi na Waziri mkuu wa Malaysia Bw. Anwar Ibrahim mjini Cairo.

Nchi mbili zimesisitiza tena haki za kujiamulia za watu wa Palestina, ikiwemo haki ya kuanzisha nchi huru.

Viongozi hao pia wamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufikiria ombi la Palestina la uanachama kamili wa Umoja wa Mataifa kutokana na azimio husika lililopitishwa na mkutano mkuu wa Umoja huo Mei 10 mwaka huu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha