Lugha Nyingine
Kiwanda cha Mataruma ya reli cha China nchini Algeria chaanza uzalishaji
(CRI Online) Novemba 11, 2024
Kiwanda kipya cha mataruma ya reli cha China kilifunguliwa jana Jumapili katika jimbo la Tindouf, magharibi mwa Algeria. Kiwanda hicho kinatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika ujenzi wa mradi wa reli kuelekea eneo la machimbo ya chuma, unaotekelezwa na kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China, CRCC.
Kiwanda hiki ni hatua ya mwanzo ya uhandisi kwa ajili ya ujenzi wa reli yenye urefu wa kilometa 575, ambayo itaunganisha eneo la machimbo ya chuma la Gara Djebilet huko Tindouf, na jimbo la wa Bechar.
Meneja mkuu wa CRCC tawi la Afrika Kaskazini Bw. Dong Lin, amesema kiwanda hicho cha mataruma, ni cha kwanza cha mataruma ya saruji kujengwa na kampuni ya China katika jimbo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma