Lugha Nyingine
Rais Xi atoa pongezi kwa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Jumuiya za Washauri Bingwa la Nchi za Kusini
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Jumuiya za Washauri Bingwa la Nchi za Kusini.
Rais Xi akidhihirisha kuwa kwa hivi sasa, mwelekeo wa maendeleo ya Nchi za Kusini ni wenye nguvu kubwa na kutoa mchango na kufanya kazi muhimu zaidi katika mambo ya maendeleo ya binadamu, China siku zote ni moja kati ya Nchi za Kusini na daima itakuwa moja kati ya nchi zinazoendelea.
Amesema China ina nia ya kufanya juhudi pamoja na Nchi za Kusini katika kufanya ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kutetea dunia yenye ncha nyingi iliyo ya usawa na utaratibu na utandawazi wa uchumi wenye manufaa na jumuishi kwa wote, na kuhimiza kwa pamoja kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Rais Xi amesisitiza kwamba kukabiliana na mabadiliko duniani ya karne hii, kutafuta ujenzi wa mambo ya kisasa na kuhimiza utaratibu wa kimataifa wenye haki na usawa ni jukumu takatifu la kihistoria la Nchi za Kusini na pia ni masuala ya pamoja ya zama hizi kwa vyombo vya habari na jumuiya za washauri bingwa za Nchi za Kusini.
Rais Xi ametumai washiriki wa jukwaa hilo watashiriki katika majadiliano ya kina, kupata maoni ya kauli moja, na kwa pamoja kupaza "sauti ya Nchi za Kusini" huku wakionyesha "dhamira ya Nchi za Kusini."
Pia amewahimiza kuchangia hekima katika kuimarisha uwezo wa Nchi za Kusini na kuziwezesha kuwa nguvu ya kuleta utulivu, uti wa mgongo wa ufunguaji mlango na maendeleo, nguvu ya kiujenzi katika usimamizi wa dunia nzima, na nguvu ya kuhimiza kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali.
Jukwaa la Vyombo vya Habari na Jumuiya za Washauri Bingwa la Nchi za Kusini limeanza jana Jumatatu mjini Sao Paulo, Brazil. Jukwaa hilo, lililoandaliwa kwa pamoja na Shirika la Habari la China, Xinhua na Kampuni ya Mawasiliano ya Habari ya Brazili, linafanyika chini ya kaulimbiu ya "Maendeleo na Ustawishaji: Safari Mpya kwa Nchi za Kusini".
Pia siku hiyo ya Jumatatu, Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva alituma ujumbe wa pongezi kwa jukwaa hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma