Lugha Nyingine
Shughuli ya kuunganisha wadau wa ushirikiano wa kuendeleza tasnia ya magari ya Henan, China yafanyika Zhengzhou
Shughuli ya kuunganisha wadau wa ushirikiano wa kuendeleza tasnia ya magari ya Henan ikifanyika. (Picha na Shen Zhiyuan/People’s Daily Online)
Shughuli ya kuunganisha wadau wa ushirikiano wa kuendeleza tasnia ya magari ya Mkoa wa Henan, China imefanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano na Maonesho cha Zhengzhou siku ya Jumamosi, tarehe 9, Novemba.
Shughuli hiyo ililenga kujenga daraja na jukwaa la mawasiliano na ushirikiano kwa wadau wa tasnia ya magari, ikiwa imeandaliwa na Idara ya Biashara ya Mkoa wa Henan na serikali ya Mji wa Zhengzhou, na kutekelezwa na Idara ya Biashara ya Mji wa Zhengzhou na Idara ya Teknolojia za Viwanda na Habari ya Mji wa Zhengzhou.
Mnamo mwaka 2023, Mkoa wa Henan uliorodhesha magari yanayotumia nishati mpya (NEVs) katika makundi ya kuwekewa mkazo wa kuendelezwa ya minyororo ya viwanda, na tangu wakati huo kiwango cha tasnia yake ya magari yanayotumia nishati mpya kimeendelea kuongezeka. Katika robo tatu za kwanza mwaka huu, mauzo ya nje ya nchi ya magari ya Mkoa wa Henan yalifikia Yuan bilioni 23, ambapo kati ya hayo magari yanayotumia umeme yalichukua Yuan bilioni 5.7.
Katika hotuba yake, Zhang Min, mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama cha Kikomunisti cha China ya Mkoa wa Henan, ambaye pia ni naibu mkuu wa Mkoa wa Henan, amesema Mkoa huo kimsingi umejenga mnyororo kamili wa viwanda vya magari kuanzia malighafi hadi sehemu muhimu za gari, na kisha hadi vifaa vinavyounda magari kamili na Intaneti ya Vitu (IoT).
Amesema kwa sasa mkoa huo umekusanya kampuni 17 za kuunda magari kamili na viwanda zaidi ya 600 vya kuunda sehemu za magari vyenye saizi kubwa.
“Katika siku za baadaye, Henan itategemea faida zake za kipekee za jiografia ya usafirishaji, saizi ya soko, rasilimali watu na msingi wa kiviwanda, kujenga msingi wa tasnia ya magari yanayotumia nishati mpya unaoongoza nchini China” amesema Zhang.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma