DPRK yaidhinisha mkataba wa ushirikiano wa kimkakati na Russia

(CRI Online) Novemba 12, 2024

Shirika la Habari la Korea (KCNA) limeripoti kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) imeidhinisha mkataba wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati yake na Russia chini ya amri ya kiongozi mkuu wa nchi hiyo Bw. Kim Jong-un.

Shirika hilo limesema Bw. Kim Jong-un amesaini amri hiyo jana Jumatatu na mkataba huo utaanza kutekelezwa siku ambayo pande hizo mbili zitabadilishana hati za kuuridhia.

Mwezi Juni mwaka huu wakuu wa nchi hizo mbili walisaini mkataba huo baada ya kukutana mjini Pyongyang.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha