Lugha Nyingine
Kenya yaanzisha mageuzi ya kuimarisha usafiri wa abiria katika uwanja mkuu wa ndege
Serikali ya Kenya imeanza mageuzi katika uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKlA) mjini Nairobi, ili kuongeza idadi ya abiria.
Waziri wa fedha na mipango ya uchumi wa Kenya Bw. John Mbadi, amesema kwenye taarifa iliyotolewa mjini Nairobi, kuwa mageuzi hayo yatatoa huduma zisizo na changamoto, zenye ufanisi na staha kwa wateja wanaoondoka na kuwasili.
Amesema serikali imeweka kipaumbele katika teknolojia ya hali ya juu kwenye mageuzi ya kuboresha taratibu za forodha na uhamiaji ili kupunguza matumizi ya karatasi.
Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ni moja ya vituo vitatu vikuu vya kuingilia nchini Kenya, sambamba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Moi mjini Mombasa, na wa Kisumu magharibi mwa Kenya.
Watalii wengi wa Kenya waliwasili kupitia JKIA, huku wengine wakiingia nchini humo kupitia uwanja wa ndege wa Moi.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya, katika robo ya kwanza ya mwaka huu, Kenya ilipokea watalii laki 4.09 kupitia viwanja hivyo viwili vya ndege, huku laki 3.43 kati ya hao wakitumia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma