Uwanja wa ndege uliojengwa na kampuni ya China mjini Luanda, Angola wapokea ndege za kwanza za abiria

(CRI Online) Novemba 12, 2024

Uwanja mpya wa ndege wa kimataifa wa Dkt. Antonio Agostinho Neto mjini Luanda, Angola uliojengwa na kampuni ya uhandisi wa teknolojia ya anga ya China, umekamilisha mapokezi ya safari za kwanza za ndege za abiria asubuhi ya Jumapili.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi ya Angola, uwanja huo ulioko umbali wa kilomita 40 kusini mashariki mwa Luanda, ulipokea ndege nne za safari za Shirika la Ndege la Angola (TAAG) kati ya Luanda na Cabinda, katika siku yake ya kwanza ya huduma za abiria.

Uwanja huo wa ndege uliosanifiwa kuwa na uwezo wa kusafirisha abiria milioni 15 na tani 130,000 za mizigo kwa mwaka, unalenga kuwa kituo kikubwa cha usafiri wa anga katika eneo la kusini mwa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha