Wapalestina 21 wauawa katika mashambulizi ya Israel huko Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2024

Mtoto mvulana akiomboleza mwathiriwa katika eneo la Mawasi la Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 12, 2024. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

Mtoto mvulana akiomboleza mwathiriwa katika eneo la Mawasi la Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 12, 2024. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

GAZA - Wapalestina takriban 21 wameuawa siku ya Jumanne katika mashambulizi ya Israel kaskazini na katikati mwa Ukanda wa Gaza, vyanzo mbalimbali vya habari vya Palestina vimesema, ambapo Mamlaka ya Ulinzi wa Raia ya Palestina mjini Gaza imesema katika taarifa fupi kwamba ndege za Israel zilipiga mabomu dhidi ya nyumba mbili katika mji wa Beit Hanoun, mbali na kaskazini mwa ukanda huo.

Madaktari wameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba shambulizi hilo limesababisha vifo vya watu wasiopungua 15, wakiwemo wanawake na watoto, na wengine wamejeruhiwa kwa hali mbalimbali tofauti.

Vyanzo mbalimbali vya habari vimeripoti kuwa, droni ya kivita ya Israel pia ilipiga mabomu dhidi ya mkusanyiko wa Wapalestina karibu na kliniki iliyo chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) magharibi mwa mji wa Deir al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Watu waliopata habari kutoka Hospitali ya Al-Aqsa mjini humo wameliambia shirika la habari Xinhua kwamba watu sita wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa, baadhi yao wamejeruhiwa vibaya.

Aidha, jeshi la Israeli lilizingira familia zipatazo 130 ndani ya vituo vitatu ambavyo vilianzishwa kwenye mahali pa shule huko Beit Hanoun na kulazimisha watu waliokuwa ndani kuondoka katika mji huo, vyanzo vya habari vya eneo hilo na mashuhuda wameeleza.

Vyanzo hivyo na mashuhuda wameliambia Xinhua kwamba watu hao waliokimbia makazi yao wameondoka kwenye vituo hivyo chini ya milio ya risasi.

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limesema katika taarifa yake siku ya Jumanne kwamba jeshi hilo linaendelea na operesheni katika eneo la Jabalia. Wiki iliyopita, wanajeshi wamekuwa wakifanya msako ili "kuondoa tishio" katika eneo la Beit Lahia, imesema taarifa hiyo. 

Mwanamke akilia kuomboleza wathiriwa katika eneo la Mawasi la Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 12, 2024. (Picha na Rizek Abdeljawad/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha